Wednesday, January 2, 2013
Jamaa wawili walikutana kwenye kituo cha
basi wakafanya mazungumzo. Mmoja
aling'ang'nia kuzungumzia kero za familia
yake hatimaye mwenzake akasema "
Unadhani familia yako ina matatizo?" Basi
sikiliza kisa changu hiki….
"Miaka michache iliyopita nilikutana na
mwanamke mjane aliyekua na binti mkubwa
tu na mimi na huyo mjane tukaamua kuoana.
Baadaye baba yangu akamuoa binti yangu wa
kambo (yaani binti wa huyu mke wangu
niliyemwoa akiwa mjane), hivyo huyo binti
yangu wa kambo akawa mama yangu wa
kambo na Baba yangu akawa mtoto wangu
wa kambo wa kiume ambapo mke wangu
akawa mama mkwe wa mkwe wake.
Baadaye binti ya mke wangu yaani binti
yangu wa kambo (ambaye kwa sasa ndiye
mke wa baba yangu na hivyo kuwa pia mama
yangu wa kambo) alipata mtoto wa kiume.
Mtoto huyo wa kiume akawa mdogo wangu
kwa sababu tulichangia baba mmoja. lakini
kwa vile pia alikua ni mtotowa binti wa mke
wangu papo hapo akawa mjukuu wa mke
wangu na mimi nikawa babu yake huyo
mdogo wangu.
Lakini hayo yote yalikua si kitu mpaka mimi
na mke wangu tulipopata mtoto wa kiume.
Sasa msichana (yaani binti ya mke wangu
ambaye pia ni mke wa baba yangu) ambaye
ni ndugu wa mtoto wangu huyo wa kiume
kwa kuchangia mama yao mmoja, akawa pia
bibi yake na mwanangu (mwee!!). Hali hiyo
ilimfanya pia baba yangu kuwa shemeji wa
mtoto wangu (achilia kuwa babu yake!!)
ambaye ndugu yake wa kike kwa upande wa
mama yao ndie mke wake baba yangu. Kwa
hiyo mimi ni shemeji yake mama yangu wa
kambo ambapo mke wangu ni mama mdogo
(anti) wa binti yakemwenyewe . Mtoto wangu
wa kiume ni mpwa wa baba yangu ambapo
mimi nikawa babu yangu mwenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment